SOMO LA USIKU,.

    YAFAHAMU MAANDIKO.

SOMO :POKEA SILAHA ILI ZIKULINDE USIKU HUU

FUNGU KUU:  ISAYA 54:17
17 Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.
    Mpendwa hebu tafakari juu ya URITHI NA HAKI  kwa watumishi wa Mungu ulivyo wa ajabu;
1.Kila silaha
   itakayofanyika juu yangu HAITAFANIKIWA
2.Kila ulimi
  utakaoinuka juu 
  yangu katika hukumu
 NITAUHUKUMU KUWA  mkosa.
    Mpendwa ni haki yako kama mtumishi wa Bwana kupata ulinzi wa Ki Mungu katika mazingira yote.
   Ulimi unaumba jambo zuri au baya. Ulimi unaotamka baya juu yangu hauna nafasi kwa jina la Yesu.
     Mungu akubariki sana, simama katika neno upokee ushindi dhidi ya silaha zote zinazorushwa juu yako.
  UWE NA USIKU MWEMA MTU WA MUNGU




Imeandaliwa na mwandishi wako
Emmanuel

Maoni

Machapisho Maarufu