SOMO LA USIKU--SOMA UPATE MAARIFA NA MIBARAKA
MADA:FAHAMU NGUVU YA MAOMBI
Kutoka kwa mwandishi wako Derick Byanit
HANA MKE WA ELIKANA
Leo tuangalie jinsi huyu mama alivyoomba na BWANA alivyojibu ombi lake.
Neno la Bwana linasema:
"Palikuwa na mtu mmoja wa Rama.......jina lake akiitwa Elikana........naye alikuwa na wake wawili;jina lake mmoja aliitwa Hana,na jina lake wa pili aliitwa Penina;naye huyo Penina alikuwa na watoto,lakini Hana hakuwa na watoto." 1Samweli 1:1,2
Huyu mama alikuwa na uchungu sana kwa sababu hakuwa na watoto na pia mke mwenzake alikuwa anamchokoza sana. Lakini aliamua kufanya maamuzi ya kuutafuta uso wa Mungu asiyeshindwa na jambo lo lote ili amueleze shida yake pale hekaluni.
Neno la Bwana linasema,"Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake,akamwomba Bwana,akalia sana. Akaweka nadhiri,akasema,Ee Bwana wa majeshi,ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako,na kunikumbuka,wala usinisahau mimi mjakazi wako,na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume,ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake......" 1Samweli 1:10,11
BWANA alisikia kilio chake.
"Ikawa,wakati ulipowadia,Hana akachukua Mimba na kuzaa mtoto mwanamume;akamwita jina lake Samweli,akisema,kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA." 1Samweli 1:20
Huyu mama alitimiza nadhiri yake kwa kumpeleka mtoto wake hekaluni kama alivyoahidi.Naomba usome 1Samweli 1:24-28.
Bwana Mungu anahitaji watu waaminifu kama yeye. Mama huyu alitimiza nadhiri yake kama alivyoahidi.
BWANA MUNGU ni mwaminifu kwa kusikia kilio cha wao wamtafutao. Ndugu zangu, huzuni ulizo nazo katika majaribu au mazingira magumu unayoyapitia,zinazokufanya machozi kutoka,kilio chako hakitapita kamwe pale utakapoutafuta uso wa BWANA ili akusikie.
Neno la BWANA linasema hivi:
"Kuna neno gani gumu la kumshinda BWANA?......Mwanzo 18:14
"Aa! Bwana Mungu,tazama,wewe umeziumba mbingu ba nchi,kwa uwezo wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa;hakuna neno lililo gumu usiloliweza." Yeremia 32:17
"Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia,kusema, Tazama,mimi ni BWANA,Mungu wa wote wenye mwilu;je kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?" Yeremia 32:26
"Niite,nami nitakuitikia,nami nitakuonyesha mambo makubwa,magumu usiyoyajua."Yeremia 33:3Yapo mambo ambayo kwayo tunaona hayawezekani lakini Mungu aliyemuumba wa vyote anasema tumuite yeye naye atatuonyesha mambo makubwa na magumu tusiyoyajua. Kuna wakati Mungu huwa anatupitisha katika changamoto mbalimbali bila sisi kujua.
Pia BWANA anasema:
"Nanyi mtaniita,mtakwenda na kuniomba,nsmi nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta,na kunioba,mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote." Yeremia 29:13,14.
NDUGU ZANGU,TUSIKATE TAMAA,TUWE NA MATUMAINI,BWANA YUPO KWA AJILI YETU. IKIWA ALISIKIA SAUTI YA HANA AKIOMBA PEKE YAKE,ATASIKIA MAOMBI YETU.
TUMWOMBE BWANA ATUONGEZEE IMANI. AMANI YA BWANA IWE PAMOJA NANYI.
Somo by Derrick Baynit
Maoni
Chapisha Maoni
THANKS FOR COMMENTING
Name:
Where are you comming from:
Mobile no.:
Comment: