SOMO LA ASUBUHI
JE WEWE WATU WAMEONA NINI ?????
KESHA LA ASUBUHI
JUMATANO-AGOSTI 23, 2017
JE,WANAONA NINI?
"Ndipo akasema, Wameona nini katika nyumba yako? Hezekia akajibu, Wameviona vitu vyote vilivyomo nyumbani mwangu; hapana kitu katika hazina zangu nisichowaonyesha." Isaya 39:4.
▶Ziara ya mabalozi kwa Hezekia lilikuwa jaribio la kuangalia hali yake ya kushukuru na kujitoa… Kama Hezekia angetumia vizuri fursa aliyopewa ili kuwa shahidi wa uwezo, wema, huruma za Mungu wa Israeli, taarifa ya mabalozi ingekuwa kama nuru inayopenya gizani. Lakini alijiinua mwenyewe juu kuliko Bwana wa majeshi. “Walakini kadiri alivyofadhiliwa Hezekia hakumrudishia vivyo; kwa kuwa moyo wake ulitukuka.”…
▶Kisa cha kushindwa kwa Hezekia kuthibitisha uaminifu wake… kimejazwa na vitisho vyenye fundisho muhimu kwa ajili ya wote. Kwa kiasi kikubwa zaidi ya namna tunavyofanya, tunahitajika kuzungumza juu ya sura za thamani katika uzoefu wetu, juu ya rehema na wema utokanao na upendo wa Mungu, juu ya kina kisicho na kifani cha upendo wa Mwokozi. Akili na moyo vinapojazwa kwa upendo wa Mungu, haitakuwa vigumu kutoa kile kinachoingia katika maisha ya kiroho. Mawazo mazuri, shauku njema, utambuzi bayana wa ukweli, makusudi yasiyo ya kibinafsi, hamu ya utauwa na utakatifu, yataonekana katika maneno yanayodhihirisha tabia ya hazina iliyo moyoni.
▶Wale tunaoshirikiana nao siku kwa siku wanahitaji msaada, uongozi wetu. Wanaweza kuwa katika hali ya kimawazo ambapo neno linalonenwa kwa wakati linaweza kuwa kama msumari uliowekwa mahali penye uhakika. Kesho, baadhi ya roho hizi zinaweza kuwa mahali ambapo hatuwezi kuzifikia tena. Mguso wetu kwa hawa wasafiri wenzetu ukoje?
▶Marafiki zako na wale wanaokufahamu wameona nini nyumbani mwako? Je, wewe, badala ya kudhihirisha hazina za neema ya Kristo, unaonesha vitu vinavyotumika na kuharibika? Au wewe, unawasiliana juu ya mawazo mapya ya tabia na kazi ya Kristo kwa wale unaokutanishwa nao?...
▶Laiti wale ambao Mungu amewatendea mambo makuu wangeonesha sifa zake na kusimulia juu ya matendo yake makuu. Lakini ni mara nyingi kiasi gani, wale ambao Mungu anawatendea wanakuwa kama Hezekia – wakisahau juu ya Mpaji wa baraka zao zote.
MUNGU AKUBARIKI
Maoni
Chapisha Maoni
THANKS FOR COMMENTING
Name:
Where are you comming from:
Mobile no.:
Comment: