SOMO LA ASUBUHI
YAFAHAMU MAANDIKO
*KESHA LA ASUBUHI*
_J"PILI 20/08/2017_
*SOMO: WAREKABI*
Yeremia 35:1-19
_📜"Naye Yeremia akawaambia watu wa nyumba ya Warekabi,… Kwa sababu mmeitii amri ya Yonadabu, baba yenu, na kuyashika maagizo yake yote,… kwa sababu hiyo, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Yonadabu, mwana wa Rekabu, hatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu hata milele." Yeremia 35:18, 19._
Mungu alimwamuru Yeremia kuwakusanya Warekabi kwenye nyumba ya Bwana, kwenye moja ya vyumba, na kuwaandalia divai na kuwakaribisha wainywe. Yeremia alifanya kama Bwana alivyomwamuru. “Wakasema, Hatutakunywa divai; kwa maana Yonadabu, mwana wa Rekabu, baba yetu, alituamuru, akisema, Msinywe divai, ninyi wala wana wenu, hata milele.”
“Ndipo neno la Bwana likamjia Yeremia, kusema,.…Enenda ukawaambie wana wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu, Je! Hamtaki kupokea mafundisho, myasikilize maneno yangu? Asema Bwana. Maneno ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, aliyowaamuru wanawe, kwamba wasinywe divai, yametimizwa, na hata leo hawanywi; maana waitii hiyo amri ya baba yao.” Hapa Mungu analinganisha utii wa Warekabi na hali ya kutotii na uasi wa watu wake, ambao hawakuwa wakipokea maneno yake ya maonyo na makaripio… Warekabi walipongezwa kwa sababu ya kuwa tayari na kuwa watiifu, wakati watu wa Mungu walipokataa kukemewa na manabii wao.
Ikiwa masharti ya baba mwema na mwenye hekima, ambaye alifanya mambo yaliyo bora sana na yenye mguso ili kuhakikisha usalama wa vizazi vyake dhidi ya uovu wa kutokuwa na kiasi, yalistahili utii makini, kwa hakika mamlaka ya Mungu yanapasa kuchukuliwa kwa kicho cha juu zaidi kwani yeye ni mtakatifu kuliko mwanadamu. Muumbaji wetu na Amirijeshi wetu, mwenye uwezo usio na kikomo, wa kutisha katika hukumu, kwa kila namna anataka awafikishe watu waone na kutubu dhambi zao. Kwa kinywa cha watumishi wake anatabiri hatari ya kutokutii; anatoa tamko la onyo na kwa uaminifu anakemea dhambi. Watu wake wanapewa mafanikio kutokana na rehema yake tu, kutokana na hali ya kuwa macho ya wale waliochaguliwa. Hawezi kuwaunga mkono na kuwalinda watu wanaokataa mashauri yake na kudharau kukemewa naye. Kwa muda fulani anaweza kuzuia hukumu zake zinazopatiliza; hata hivyo, hawezi kuzuia mkono wake siku zote.
➕➕➕➕🙏🏾🙏🏾🙏🏾➕➕➕➕
*UBARIKIWE*
Maoni
Chapisha Maoni
THANKS FOR COMMENTING
Name:
Where are you comming from:
Mobile no.:
Comment: