SOMO LA ASUBUHI
. .YAFAHAMU MAANDIKO
Mshukuru mungu kwa ulinzi wake usiku wote mpaka umeamka salama
๐ฑ ๐ฆ
๐ฆ ๐ธ ๐บ ๐ง ๐บ ๐ญ
๏ผญ๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ/
๏ผฉ๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ 18/08/2017
๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ... ๐๐ฝ๐๐ฝ๐๐ฝ
๐ฐ ๐ผ ๐ฆ
๐ฆ ๐ฏ ๐ฎ ๐ฑ ๐ฎ
๐พ ๐ฆ
๐ฐ ๐ฎ ๐ฑ ๐ฆ ๐ฒ ๐น ๐บ
*_✍๐ฝ๐Masheki watakuja kutoka Misri, Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara. Zaburi 68:31._*
____________________________
*๐ฐatika huduma yake yote, Isaya alikuwa na ushuhuda wazi kuhusu kusudi la Mungu kwa ajili ya wamataifa. Manabii wengine walikuwa wametaja kuhusu mpango huu wa Mungu, lakini siyo sikuzote lugha yao ilieleweka. Isaya alipewa jukumu la kuweka wazi kwa Yuda ukweli kwamba kati ya Israeli wa Mungu ilipasa wawepo wengi ambao hawakuwa wazao wa Ibrahimu kimwili. Fundisho hili halikupatana na teolojia ya wakati wake, hata hivyo, alihubiri ujumbe huu aliopewa na Mungu bila hofu na hivyo kuleta tumaini kwa wengi ambao mioyo yao ilikuwa na shauku ya kufikia baraka za kiroho zilizoahidiwa kwa wazao wa Ibrahimu…*
*๐ฒara kwa mara Waisraeli walionekana kutokuwa na uwezo au kutokuwa tayari kuelewa kusudi la Mungu kwa wamataifa. Licha ya hivyo, hili lilikuwa ndilo kusudi lililowafanya kuwa watu waliotengwa na kuwaanzisha kama taifa huru kati ya mataifa ya dunia. Ibrahimu, baba yao, ambaye ndiye aliyepewa ahadi ya agano kwanza, alikuwa ameitwa kutoka kwa watu wake, kwenda kwenye eneo la mbali, ili apate kuwa mbeba nuru kwa wamataifa. Japo ahadi aliyopewa ilihusisha vizazi kwa wingi kama mchanga wa bahari, kuwa kwake baba wa taifa kuu hakukufanyika kwa sababu za kibinafsi…. Yehova alitamka, “Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako;… na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.”…*
*๐ฒungu hatambui ubora wa mmoja kuliko mwingine kulingana na utaifa, rangi, au ukoo….Kristo alikuja kuvunja kila ukuta unaotenganisha, kufungua kila chumba cha nyua za hekalu, ili kila nafsi iwe na uhuru wa kumfikia Mungu. Upendo wake ni mpana sana, una kina kirefu, ni mkamilifu kabisa kiasi cha kuweza kupenya kila mahali. Unatoa wale walio nje ya mvuto wa Shetani, wale ambao wameghilibiwa na udanganyifu wake na kuwaweka karibu na kiti cha enzi cha Mungu, kiti cha enzi ambacho kimezingirwa na upinde wa ahadi. Katika Kristo hakuna Myahudi wala Myunani, mtumwa wala huru.*
.....
Tafakari ..njema
...
Maoni
Chapisha Maoni
THANKS FOR COMMENTING
Name:
Where are you comming from:
Mobile no.:
Comment: