SOMO LA ASUBUHI
NYEUPE KAMA THELUJI
-unajua ni nini?
-karibu katika somo hili
๐ฐ ๐ช ๐ธ ๐ญ ๐ฆ ๐ฑ ๐ฆ
๐ฆ ๐ธ ๐บ ๐ง ๐บ ๐ญ ๐ฎ
๏ผก๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ ......
๏ผก๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ๏ฝ.17/2017
Somo.... ๐๐ฝ๐ฐ
๐ณ ๐พ ๐ช ๐บ ๐ต ๐ช
๐ฐ ๐ฆ ๐ฒ ๐ฆ
๐น ๐ญ ๐ช ๐ฑ ๐บ ๐ฏ ๐ฎ
____________________________
✍๐ฝ๐Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu. Isaya 57:15.
๐ฐwenye ile njozi iliyomjia Isaya ndani ya nyua za hekalu, alioneshwa mwonekano dhahiri wa tabia ya Mungu wa Israeli. “Yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu,” alikuwa amemtokea katika ukuu wa ajabu; licha ya hivyo, nabii alieleweshwa juu ya silika ya Bwana ya rehema….
๐ฐwa kumtazama Mungu, huyu nabii …. si tu kwamba alipewa kuona hali yake ya kutokufaa; bali pia ndani ya moyo wake ulionyenyekezwa aliletewa uhakika wa msamaha, uliokuwa kamili na wa bure; hivi akainuka akiwa mtu aliyebadilika. Alikuwa amemwona Bwana. Alipata mwonjo wa uzuri wa tabia ya kimbingu. Sasa angeweza kushuhudia juu ya badiliko linalofanywa kwa njia ya kutazama Pendo Lisilo na Kikomo. Kuanzia hapa na kuendelea, alivuviwa kwa shauku kali ya kuona Israeli iliyokosa ikiwekwa huru kutoka katika mzigo na adhabu ya dhambi. Nabii huyu akahoji, “Mbona mnataka kupigwa hata sasa?.…Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.”… Mungu waliyedai kumtumikia, lakini ambaye tabia yake hawakuielewa, aliwekwa mbele zao kama Mponyaji mkuu wa ugonjwa wa kiroho…
๐ฒoyo wa yule Mwenye Upendo Usiokoma anatamani wale wanaojisikia kutokuwa na nguvu ya kujiweka huru kutoka kwenye mitego ya Shetani; naye kwa rehema huwapa nguvu ya kuwawezesha kuishi kwa ajili yake. Anawaambia, “Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.”…
๐ฏe, wewe msomaji, umechagua njia yako mwenyewe? Umetanga mbali na Mungu? Umejaribu kujilisha matunda ya uasi, ukashangaa yakigeuka kuwa majivu midomoni mwako? …. Rejea nyumbani kwa Baba yako. Yeye anakukaribisha, akisema, “Unirudie; maana nimekukomboa. Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi.”
:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
TAFAKARI
..... chukua HATUA.. ๐๐ฝ
Maoni
Chapisha Maoni
THANKS FOR COMMENTING
Name:
Where are you comming from:
Mobile no.:
Comment: