FAHAMU MAANA YA MUZIKI

  1.   HIVI MUZIKI NI NINI HASA?
  1. 

  1. Muziki ni sanaa kama zilivyo sanaa zingine, hivyo hatuna budi kuelewa sanaa ni nini hasa. Imeelezwa kuwa ni ufundi wa kuwasilisha mawazo yaliyomo katika fikra za binadamu ili yadhihirike na kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa walengwa-sanaa hiyoo.
  2. 
  3. **************************************************** 

  4.  

  5. Hivyo sanaa inabaki kuwa na malengo makuu ambayo ni kuelimisha, kuonya, kuburudisha na hata kuelekeza jamii. Sanaa pia ni utambulisho wa jamii husika. Kupitia sanaa unaweza kuifahamu jamii kuwa huu ni fulani hata kama hujawahi kuishi na jamii hiyo. 

  6. Sanaa inayo matawi mengi mno, lakini kwa leo naomba tujikite zaidi katika tawi la muziki. 

  7. Muziki ni nini hasa? 
  8. Kwa mujibu wa kamusi sanifu ya Kiswahili, muziki umeelezwa kuwa ni “mpangilio wa ala na uimbaji unaoleta athari fulani kwa kiumbe”. Hii ina maana kuwa kama msanii wa muziki hapangilii ala zake na kuimba kwa ustadi basi, anachokifanya msanii huyo si muziki bali ni kelele za kawaida. 

  9. Si nia yangu kufundisha muziki kupitia makala haya, isipokuwa ninataka tutafakari ni kwa namna gani wasanii wetu wa muziki wanavyoshiriki katika jitihada za kuleta maendeleo katika taifa letu na pia kuipotosha jamii. 

  10. Tutafanya makosa endapo tutaisahau sekta hii ya sanaa ya muziki katika ujenzi wa jamii yoyote. 

Maoni

Machapisho Maarufu