AMKA NA SOMO HILI

JE WAJUA VITU VIZURI NDIVYO VINAVYOTUTENGANISHA NA MUNGU??????

Karibu kwa somo zuri la leo lililoandaliwa na Nipael Samwel

Mara Nyingi Vile Vitu Vitakavyokufanya Ukosane na Mungu au utoke kwenye Uwepo wake doesn't have to be UGLY. Vinaweza kuwa Vizuri, Handsome, beautiful, Vina shape namba nane, Body six pack, Mguu wa bia, ni wife material, vinajua kucare, Vimesoma, Vina pesa, nk...


And the Fact that it's not Ugly doesn't mean that God approves of it.


1SAMWEL 15:3,9
Ukisoma Mstari wa 3, Mungu anamwambia Sauli akaangamize KILA Kitu, Mstari wa 9, Badala ya Saul Kuangamiza Vibaya, Yeye akajibakizia vile alivyoona ni vizuri....

Kilichotokea Alipoteza UFALME,

Unajua hata wale askari wake wangemuona Sauli kuwa Ni zuzu kama Angekubali kuangamiza vyote hata vile vzuri vizur na vitamu vitamu, Kama wewe Unavyoonekana zuzu kwa Kumkataa Huyo Pedeshee( Kijana mwenye mapesa mengi) au Mume wa mtu mwenye pesa na Serikali ya Magu hii Inavyobana...

SIKIA!!
Kitu Kinaweza kuwa Kinakupendeza lkn kama MUNGU AMESHAPIGA MUHURI WA HAPANA, hakitabadilika kiwe Chema mbele zake na Kwa Maisha Yako Kitakuangamiza tuu... Ndio maana Hata Tunapotaka Wachumba Ni Lazima Tuombe kwanza Kwa Mungu Na Tusikie Jibu Kutoka Kwake ndio au Hapana na Sio Kulazimishaa...

Hatuna Sababu ya Kupoteza Kesho Yetu kwa Sababu ya Pesa Alizonazo mtu au kazi aliyo nayo mtu au Kipaji au Uwezo alionao mtu au kitu chochote kile,Kwa Maana Siku hivyo vyote Vikitafunwa na Kutoweka ndipo Tutaelewa Nn Maana Ya Saul Kupoteza UFalme..

KAA MBALI NA MTI AMBAO MUNGU AMEKUKATAZA NA KUKUZUIA USILE MATUNDA YAKE HATA KAMA UNAVUTIA KIASI GANI, KAAA MBAALI... ( Kaa mbali na Dhambi y Uzinzi, Uongo, Usengenyaji, Kutembea na Mume au mke wa mtu, Kungang'aniza kuwa na kijana ambaye Mungu Amekataa)


Maana Kwenye Hichohicho Ulichokatazwa ndio na Nyoka anazungukia hapohapo akushawishi Ule,

Adui kamwe hakai kwenye vile Ulivyoruhusiwa Kula( mke, mume, kipato halali, mchumba sahihi nk)

Anakaa kwenye vile Ulivyonyimwa Usile( Kimada, Rushwa nk)

Anakusubiri ule tu ili Ulinzi wa Mungu Ukukimbie na AKUMALIZE.

ASUBUHI HII  SOMO HILI LINATUKUMBUSHA TUKAE MBALI WAPENDWA!!

MUNGU ATUPE NURU!! Barikiwen

Maoni

Machapisho Maarufu